• Breaking News

    Tuesday, May 24, 2016

    CANAVARO AWABEBA SIMBA

    Nahodha na kiongozi wa wachezaji wa Yanga uwanjani NADIR HAROUB "CANAVARO", ametamka jambo ambalo mashabiki wa Yanga huenda wakalitafsiri kama ni uungwana. Amesema kutokana na timu yao kuwa na majukumu ya kucheza mechi za makundi za Kombe la Shirikisho Afrika, haoni sababu ya kushiriki Kombe la Kagame kwa mwaka huu na ikibidi Simba apewe tu nafasi hiyo. Kagame itachezwa Dar es Salaam mwezi ujao ingawa bado tarehe kamili ilikuwa haijatajwa.

    Yanga inatakiwa kushiriki Kombe la Kagame mwaka huu kwa kuwa ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, huku Azam ikishiriki kama bingwa mtetezi. Kama Tanzania itakuwa mwenyeji huenda ikapata nafasi ya kushirikisha timu tatu.

    Cannavaro alisema kama Yanga itashiriki mashindano hayo wachezaji watakosa muda wa kupumzika hivyo kujiweka katika mazingira magumu ya kufanya vizuri katika mashindano hayo ya Afrika.

    “Sidhani kama tuna sababu ya kushiriki Kombe la Kagame mwaka huu kutokana na ugumu wa ratiba yenyewe, wachezaji hatutapata muda wa kupumzika. Nadhani viongozi wana haja ya kulitazama hili, kama inawezekana hiyo nafasi apewe Simba,” alisema Cannavaro ambaye ndiye mchezaji aliyekaa muda mrefu sana ndani ya Yanga miongoni mwa kikosi cha sasa.

    Kwa upande wake kocha wa timu hiyo, Hans Van Pluijm alisema wachezaji wake wanatakiwa kupata angalau mwezi mmoja wa kupumzika, lakini kulingana na ratiba ya Kombe la Kagame hilo halitawezekana.

    “Wachezaji wanatakiwa kupata angalau mwezi mmoja wa kupumzika, nadhani Kombe la Kagame linazuia nafasi hiyo, viongozi wanatakiwa kulitazama hilo,” alisema Pluijm, kocha aliyeweka rekodi ya kuiingiza Yanga katika makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.


    Contacts:
     E-mail: -
    mwamunyimalecela@gmail.com
     Facebook:- malecela mwamunyi
     Google+:- malecela mwamunyi
     whatsapp:- 0758427270

    No comments:

    Post a Comment

    PAGES

    AUDIO (5) General (1) HABARI (6) michezo (11) UDAKU (1)