• Breaking News

    Thursday, May 19, 2016

    EDO KUMWEMBE ALITAMANI HILI KWA YANGA NA LIMETIMIA

    Waswahili husema maneno huumba inawezekana ikawa kweli,Kauli hii imedhihirika baada ya mchambuzi wa soka Tanzania Edo Kumwembe kuchambua kuwa Yanga kuchukua ubingwa sio habari bali habari kuingia hatua ya makundi.

    Kiu ya mashabiki wa Dar Young Africans kuona timu yao inaingia hatua ya makundi imekamilika baada ya kufanikiwa kupita katika hatua hiyo kwenye kombe la shirikisho la soka barani Afrika.

    Yanga ilifanya vizuri mchezo wa kwanza  uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kwa ushindi wa mabao 2-0 na leo imefungwa goli 1-0 lakini goli hilo halija wasaidia Sagrada kwani Yanga imevuka kwa jumla ya mabao 2-1.

    Yanga wameonekana kuwa watamu kama asali msimu huu kwa kuchukua ubingwa wa ligi na leo hii imepita hatua ya makundi itakutana na  wakimataifa wenzake kama vile TP Mazembe ambao wameingia hatua ya makundi. Wiki inayofuata watacheza fainali ya FA dhidi ya Azam.

    No comments:

    Post a Comment

    PAGES

    AUDIO (5) General (1) HABARI (6) michezo (11) UDAKU (1)