Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection Madee amefunguka na kueleza ni kwanini wasanii wengi wa muziki wa Hip Hop nchini wanashindwa kufanya vizuri licha ya nyimbo zao kupendwa mitaani.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo, Migulu Pande, ameiambia Times Fm kuwa Hip Hop inapendwa na kundi la ‘wahuni’ wachache na machizi mtaani ambao ni ngumu kwenda dukani kununua kazi anayoipenda.
Katika hatua nyingine, Mdee amesema kama yeye angeendelea kudumu na staili yake ya kurap kama zamani mpaka sasa, angekuwa amekwisha potea kwenye ‘Game’ na ulimwengu wa muziki.
“Watu wanataka changes, kama biashara haikulipi kwanini uendelee kufanya inakuingizia hasara kila kukicha, ningekuwa narap mpaka leo nisingekuwepo kwenye game ningepotea, dunia yenyewe inabadilika sasa kwa nini wewe usibadilike” alisema Madee.
No comments:
Post a Comment