• Breaking News

    Thursday, May 19, 2016

    MICHEZO: BAADA YA KUBEBA NDOO YA EUROPA, HIZI NI REKODI KUBWA TANO (5) ZILIZOVUNJWA NA SEVILLA



    Hatimaye fainali ya michuano ya Europa League imefanyika usiku wa kuamkia leo na klabu ya Sevilla – mabingwa watetezi wa michuano hiyo, wamefanikiwa kutetea ubingwa wao mbele ya Liverpool kwa ushindi wa 3-1. 
     Magoli mawili ya Coke na moja ya Kelvin Gameiro yalitosha kuipa ubingwa wa tano wa Europa klabu hiyo ya Hispania. Ushindi huo pia umechangia kuandikwa kwa rekodi tano mpya kwenye soka la ulaya.
    1. Timu ya kwanza kubeba kombe la UEFA Cup/UEFA Europa League miaka 3 mfululizo.
      Kikosi cha Luis Molowny Real Madrid kilishinda ubingwa wa michuano hii kwenye misimu ya 1984/85 na 1985/86, na Sevilla tayari wameshaifikia rekodi ya wahispania wenzao mara mbili misimu ya 2005/06 na 2006/07, wakati Juande Ramos akiwa kocha wa timu hiyo, mara ya pili ikawa msimu wa 2013/14 na 2014/15 chini ya Unai Emery. Hakuna timu iliyoshinda michuano mikubwa ya UEFA mara 3 mfululizo – Sevilla sasa wamefanikiwa kuiweka rekodi hiyo kwa mara ya kwanza.
    2. Spain ndio nchi yenye mafanikio zaidi kwenye michuano hii. 
      Mpaka kufikia jana kabla ya mechi ya fainali, Spain na Italy kupitia vilabu vyao walikuwa wameshachukua makombe 9 kila mmoja – huku Serie A wakitoa washindi wa pili mara 6 huku La Liga wakitoa washindi wa pili 5. England (wameshinda kombe la UEFA mara 7), Germany (6) na Uholanzi (4) – Baada ya fainali ya jana, Spain sasa ndio wanakuwa nchi iliyobeba kombe hili mara nyingi zaidi.
    5. Sevilla imekuwa timu ya kwanza kubeba kombe mara 5. 
      Sevilla walifanikiwa kuwa timu ya kwanza kubeba taji hili mara ya miezi 12 iliyopita na leo wamekuwa timu ya kwnza kutimiza idadi ya makombe matano ya Europa League.  Wapinzani wao wa fainali ya jana ni moja ya timu ambazo zimebeba kombe hili kwa mara 3 1972/73, 1975/76 na msimu wa 2000/01. Washindi wengine wa mara 3 ni  Internazionale Milano (1990/91, 1993/94, 1997/98) na Juventus (1976/77, 1989/90, 1992/93).
    3. José Antonio Reyes amekuwa mchezaji wa kwanza kubeba taji hili mara 4 ndani ya fainali 4. 
      Mchezaji huyu wa zamani wa Arsenal, hivi sasa ana miaka 32, alicheza katika fainali ya ushindi wa Atletico mwaka 2010, kisha akaitumikia Sevilla katika fainali za 2014 na 2015, rekodi ambayo ilikuwa sawa na wachezaji Ray Clemence, Giuseppe Bergomi na Nicola Berti – ushindi wa fainali ya leo akiwa mchezaji wa akiba umemfanya mhispaniola huyu kuwa mchezaji aliyevaa medali nyingi zaidi  kombe la UEFA – mara 4 ndani ya fainali 4.
    5. Unai Emery amekuwa kocha wa kwanza kufikia rekodi ya kutwaa makombe matatu mfululizo na akiwa kwenye timu moja. 
      Ni Giovanni Trapattoni tu (Juventus 1976/77, 1992/93;  Internazionale Milano 1990/91) ambaye alifanikiwa kutwaa mataji matatu ya UEFA. Mpaka kufikia jana Emery alikuwa sawa na Juandr Ramos, Molowny na Rafa Benitez (Valencia 2003/04, na Chelsea 2012/13) kwa kutwaa makombe mawili ya michuano hii. Usiku wa jana Emery amekuwa kocha wa kwanza kuifikia rekodi ya Trapattoni lakini yeye ameshinda makombe yake matatu akiwa na klabu moja.  

    No comments:

    Post a Comment

    PAGES

    AUDIO (5) General (1) HABARI (6) michezo (11) UDAKU (1)