• Breaking News

    Sunday, May 8, 2016

    MICHEZO: JAMES RODRIGUEZ ATAWEKA HISTORIA UEFA

    Miaka 6 sasa imepita tangu nchi ya Colombia ambayo imejaaliwa kutoa vipaji vingi vya soka ulimwenguni – kuwa na mchezaji mwakilishi katika fainali ya michuano ya Champions League. Katika dimba la Santiago Bernabeu mnamo 2010, mchezaji wa Inter Milan Ivan Cordoba aliiwakilisha nchi yake ya Colombia katika fainali ya Inter vs Bayern. 
    14623976191372
    Jioni ya siku kikosi cha Jose Mourinho kiliwafunga Bayern Munich na kubeba ubingwa shukrani kwa magoli mawili ya Diego Milito, Cordoba alikuwa kwenye benchi la Inter akiwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumika siku hiyo. Cordoba alifanikiwa kuipata nafasi hiyo baada ya misimu 12 na Inter, na mpaka kufikia Jumatano iliyopita ndio alikuwa mchezaji pekee wa Colombia kuwahi kushiriki kwenye fainali ya Champions League. James Rodriguez sasa anakuwa mchezaji wa pili wa Colombia kuwa katika kikosi ambacho kitacheza fainali ya ulaya. 
    Msimu wa kwanza wa James na Los Blancos ulikuwa wa mafanikio kiasi, Madrid walifika nusu fainali ulaya na alicheza mechi nyingi katika mashindano yote ya ndani na nje. 
    Msimu huu mambo yamekuwa sio mazuri sana upande wake, lakini kwa uhakika atakuwa miongoni mwa kikosi kitakachochaguliwa kuhusika na mchezo wa fainali dhidi ya Atletico Madrid na hatimaye kukamilisha rekodi mpya kwa wachezaji kutoka Colombia. 

    No comments:

    Post a Comment

    PAGES

    AUDIO (5) General (1) HABARI (6) michezo (11) UDAKU (1)