• Breaking News

    Tuesday, May 31, 2016

    TAMBWE AONYWA KUHUSU SIMBA



    Siku chache baada ya mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe kudai kuwa kama uongozi wa Simba utamuomba radhi kwa mabaya yote uliyomfanyika wakati akiitumikia klabu hiyo anaweza akarejea klabuni hapo, familia yake imemuonya kuachana kabisa na suala la kuizungumzia Simba. 

    Tambwe, ambaye ndiye Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 21, ametakiwa na familia yake kufuta ndoto za kurudi Simba. 

    Tambwe alisema kuwa baada ya wazazi wake kusikia hivyo, wamemuonya na kusema kuwa Yanga ndiyo sehemu sahihi kwake kwani anaishi kwa amani bili ya masimango yoyote tofauti na alivyokuwa Simba. 

    “Wameniambia kuwa hawataki kusikia kitu chochote kinachohusiana na Simba ila wanataka kusikia mambo ya Yanga. 

    “Waliniambia kuwa walikasirika sana kusikia habari hizo, nikawaambia kuwa sikuwa namaanisha kuwa nataka kurudi Simba kwa sasa. 

    “Nilichokuwa namaanisha ni kwamba kama itafikia siku Yanga wakaamua kuniacha halafu Simba wananihitaji kwa wakati huo, basi watatakiwa kuniomba msamaha kwanza kwa yale yote mabaya waliyonifanyia nilipokuwa klabuni hapo ndipo niweze kujiunga nao,” alisema. 

    No comments:

    Post a Comment

    PAGES

    AUDIO (5) General (1) HABARI (6) michezo (11) UDAKU (1)