• Breaking News

    Thursday, June 9, 2016

    MAMBO 10 USIYOYAJUA KUHUSU BEKI MPYA WA MAN U (BAILLY)

    Bailly
    Manchester United chini ya kocha wao mpya Jose Mourinho imeanza rasmi kazi ya usajili kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi na michuano mbalimbali. Jana United walikamilisha usajili wao kwanza baada ya kumsajili beki Mu-Ivory Coast kutoka Villareal ya nchini Uhinspania Eric Bailly kwa ada ya paundi milioni 30.
    Bailly mwenye miaka 22 ni beki mwenye stamina, uwezo na anayeweza kumudu kucheza karibu nafasi zote za nyuma, anatarajiwa kuwa msaada mkubwa hasa ukizingatia kuwa kwa kipindi kirefu sasa ndiyo udhaifu ambao umekuwa ukiisumbua United.
    Hapa tunakuwekea dondoo kumi muhimu za kufahamu juu ya mchezaji huyo.
    • Kwa mara ya kwanza Bailly alinaswa kwenye rada na skauti wa Espanyol Emilio Montagut katika michuano ya vijana iliyoandaliwa na kampuni ya Promoesport ya nchini Uhipsania iliyofanyika nchini Burkina Faso.
    • Bailly alijiunga na Espanyol Desemba 2011 akiwa na umri wa miaka 17, lakini hakuwahi kupata nafasi ya kucheza mpaka Oktoba mwaka 2014, ndipo alipocheza kwa mara ya kwanza.
    • Bailly ni beki mahiri na anayetumia akili nyingi na nguvu ambaye anapenda kutembea na mpira. Kwenye michunao ya Afrika akiwa na timu yake ya taifa ya Ivory Coast alichezeshwa kama beki wa kushoto.
    • Bailly alikuwa moja ya wachezaji muhimu katika safu ya ulinzi ya kikosi cha Villareal ambacho kilipata clean sheets 17 katika msimu wa ligi wa 2015-16, waliruhusu mabao 38 katika michezo 38.
    • Bailly alikuwa ndiye mchezaji kijana zaidi katika kikosi cha Ivory Coast kilichotwaa ndoo ya Afrika mwaka 2015. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kujumuishwa.
    • Katika maisha yake yote ya soka nchini Uhispania, Bailly amecheza michezo 35 tu kunako La Liga.
    • Bailly anakuwa mchezaji wa kwanza raia wa Ivory Coast kucheza katika klabu ya Manchester United.
    • Bailly alizaliwa Ivory Coast katika mji wa Bingerville, mahali ambapo pia alizaliwa mshambuliaji wa Manchester City Wilfried Bony.
    • Akiwa amenunuliwa kwa ada ya paundi milioni 30, Bailly anakuwa beki ghali zaidi kuwahi kusajiliwa na Manchester United katika historia ya klabu hiyo. Rio anashikilia nafasi ya pili baada ya kununuliwa kwa ada ya paundi milioni 29 kutoka Leeds United mwaka 2002. Luke Shaw wa tatu baada ya kununuliwa kwa ada ya paundi milioni 27 kutoka kwa Watakatifu wa Southampton mwaka 2014.
    • Ujio wa Bailly kwenye klabu ya Manchester United unatimiza idadi ya wachezaji nane waliozaliwa Afrika kuichezea klabu hiyo. Wengine ni Patrice Evra, Nani, Wilfried Zaha, Eric Djemba-Djemba, Mame Biram Diouf na Manucho.

    No comments:

    Post a Comment

    PAGES

    AUDIO (5) General (1) HABARI (6) michezo (11) UDAKU (1)