Nigeria wamepata pigo baada ya taarifa kwamba Stephen Okechukwu Keshi aka ‘the Boss’ amefariki ghafla mapema leo asubuhi.
Mchezaji huyo wa zamani ambaye pia alimpoteza mkewe Kate mwaka jana aliyekuwa na umri wa miaka 33, kwa ugonjwa wa kansa, inaarifiwa amekufa kutokana na matatizo ya moyo huko Benin, Edo State.
Kwa mujibu wa wanafamilia na marafiki zake wa karibu, Keshi hakuonesha dalili zozote za kuumwa. Alikuwa akiishi na watoto wake wanne pamoja na mama yake mzazi.
Mwaka 2013 aliweka rekodi baada ya kuipa Nigeria kombe la Mataifa ya Afrika na kuwa kocha pekee mzawa kufanya hivyo. Pia anashilikilia rekodi ya kuwa kocha wa pili kushinda kombe hilo akiwa kama mchezaji na baadaye kocha.
Mtu mwingine aliyeweza kufanya hivyo ni Mahmoud El-Gohary wa Misri.
Aliiwakilisha Nigeria kuanzia mwaka 1982, akiwa na umri wa miaka 20, mpaka mwaka 1994, mara nyingi aliitumikia Nigeria kama nahodha na kufunga magoli muhimu hasa ukizingatia nafasi yake aliyokuwa akicheza, kama beki wa kati.
Vile vile aliwahi kuifundisha Togo na Nigeria katika kombe la dunia, vilevile Mali.
No comments:
Post a Comment