Wananchi wa Wilaya za Kilosa, Kilombero na Ulanga mkoani Morogoro, bado wanasumbuliwa na ugonjwa wa usubi, Kutokana na hali hiyo, elimu kwa jamii ya kumeza dawa hizo inatakiwa kupewa kipaumbele ili kutibu ugonjwa huo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Jacob Frank, alisema hayo mwishoni mwa wiki mjini Morogoro kabla ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa huo, Dk Stephen Kebwe kufungua semina ya uraghibishaji na uhamasishaji magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Semina hiyo iliwashirikisha wakuu wa wilaya zote za mkoani, wenyeviti wa halmashauri za wilaya, waganga wa wilaya, maofisa elimu na waratibu wa magonjwa hayo, Mganga Mkuu wa Mkoa alisema, pamoja na kupungua usubi, bado mkoa wa unasumbuliwa na ugonjwa huo hasa katika wilaya za Kilosa, Kilombero na Ulanga na uhamasishaji unaendelea kwa ajili ya kumeza dawa.
Licha ya usubi, alisema ugonjwa wa vikope ulikuwa katika wilaya za Kilosa na Gairo, lakini kutokana na juhudi za pamoja, maambukizi yake yamedhibitiwa na hivyo ugonjwa huo kutokomezwa, Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Mkoa wa Morogoro, Dk Debora Kabudi alisema baadhi ya maeneo bado wananchi wanaugua magonjwa hayo. Dk Kabudi alisema hali hiyo inatokana na baadhi yao kutomeza dawa zinazotolewa katika mpango wa kutokomeza magonjwa hayo.
Alisema tayari mpango wa kuhamasisha wananchi katika kumeza dawa ili kufikia asilimia 80, pia umelenga kuwahimiza viongozi hao kushiriki vyema mpango huo. Mkuu wa Mkoa huo alisema, ni aibu kwa wananchi kuendelea kuugua vikope, kichocho na minyoo ya tumbo, wakati serikali inatoa dawa zake bure kila mwaka.
No comments:
Post a Comment