Kupitia account yake ya mtandao wa twitter,staa wa miondoko ya Afro-Pop ambae pia ni Host wa show ya “Lip Sync” inayorushwa na kituo cha televisheni cha MTv,D’Banj amedai kuwa yupo mbioni kuifikisha mahakamani moja ya kampuni inayomiliki mtandao wa simu nchini Nigeria kwa madai ya kampuni hiyo kujinufaisha kibiashara kupitia kazi zake za kisanaa bila kuzingatia makubaliano na hakimiliki ya kazi hizo.
Hata hivyo kampuni inayotuhumiwa na Mwanamuziki huyo inatajwa kuwa ni Globacom,kampuni ambayo D’Banj alikua balozi wake ambapo tangu mkataba wake ulipoisha kama balozi wa mtandao huo,hajasaini mkataba na kampuni nyingine.
Hatua ya Mwanamuziki hiyo imekuja ambapo pia tarehe 4 ya mwezi May mwka huu,alitangaza kusitisha mkataba wake kama balozi wa kinywaji cha “Ciroc Vodka”huku tetesi zikidai kuwa yupo kwenye mpango wa kuzindua brand ya kinywaji chake binafsi.
______________________________
Contacts us:
E-mail: - mwamunyimalecela@gmail.com
Facebook:- malecela mwamunyi
Google+:- malecela mwamunyi
whatsapp:- 0758427270
No comments:
Post a Comment