1999
Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya si tu ni moja ya matukio yenye mvuto wa aina yake Ulaya bali ulimwenguni kwa ujumla kutokana na kujumuisha wachezaji wenye majina makubwa katika ulimwengu wa soka.
Kuanzia fainali ya mwaka 1999 ambapo United walitoka nyuma na kubeba ndoo dhidi ya Bayern, maajabu ya Liverpool Istanbul mwaka 2015 dhidi ya AC milan, John Terry kukosa penati fainali ya mwaka 2008 na mpaka ushujaa wa Didier Drogba mwaka 2012 Alianz Arena dhidi ya Bayern, utaona kwamba Ligi ya Mabingwa Ulaya imekuwa ikitoa matokeo yenye msisimko wa aina yake kutokana na hali ya sintofahamu inayotokea katika nyakati tofauti.
Hizi hapa ni fainali tano za UEFA Champions League ambazo zimewahi kuwa na matokeo ya aina yake.
Fainali ya Real Madrid CF v Bayer 04 Leverkusen, 2001/02
Shuti la hewani la Zinedine Zidane kwa kutumia mguu wa kushoto lilitosha kuwapa Real Madrid ubingwa baada ya kuwafunga Bayer 04 Leverkusen. Katika mchezo huo wa fainali uliopigwa katika dimba la Hampden Park jijini Glasgow nchini Scotland mwaka 2012, Real ilishinda mabao 2-1.
Bayern Munich v Chelsea, fainali mwaka 2011/12
Msimu wa UEFA mwaka 2011/12, Chelsea walishinda taji lao la kwanza la UEFA baada ya kuwafunga kwa matuta Bayern Munich katika dimba la Allianz Arena, shukrani za pekee ziende kwake Didier Drogba ambaye alikuwa shujaa wa mchezo.
Bayern walikuwa katika harakati za kushinda taji lao la nne la UEFA ambapo bao la kichwa la dakika za mwisho la Thomas Mueller liliwapa matumaini ya kutwaa ndoo kabla ya Didier Drogba kuisawazishia Chelsea dakika mbili kabla ya mchezo na kuupeleka mchezo dakika 120 na baadaye matuta.
Kwenye matuta, Drogba alipiga penati ya mwisho ambayo ndiyo iliwapa Chelsea ubingwa.
Liverpool FC v AC Milan, faina ya mwaka 2004/05
Hii wenyewe wanaita ‘‘Miracle of Istanbul’’ (maajabu ya Istanbul). AC Milan walikuwa mbele kwa magoli 3-0 mpaka kipindi cha kwanza kinaisha lakini Liverpool walirudi kipindi cha pili na kasi ya aina yake na kurudisha mabao yote matatu na kuupeleka mchezo katika muda wa ziada.
Baada ya hapo, Liverpool walishinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati na huku shujaa wa mchezo akiibuka kuwa Jerzy Dudek, mlinda mlango wa zamani wa Liverpool.
Chelsea v Manchester United, fainali ya mwaka 2007/08
Kiukweli John Terry yupo ni kipenzi cha mashabiki wengi wa Chelsea lakini kwa hili la kukosa penati muhimu kamwe hawatamsahau. Hii ilikuwa ni fainali dhidi ya Manchester United iliyopigwa Moscow nchini Urusi.
Baada ya sare ya bao 1–1 na mchezo kwenda muda wa ziada na hatimaye penati, Cristiano Ronaldo alikosa penati ya tatu kwa upande wa Manchester United na nahodha huyo wa Chelsea alikuwa akipiga penati iliyokuwa ikiwapa kombe lakini kwa bahati mbaya aliteleza na kupiga mpira ambao uligonga mwamba.
Mlinda lango wa Manchester United wakati huo Edwin van der Sar aliokoa penati ya Nicolas Anelka ambayo ilikuwa ni ya saba na kuwapa United taji la UEFA kwa mara ya tatu.
Manchester United v FC Bayern MĂĽnchen, fainali ya mwa 1998/99
Bayern Munich walikuwa wakiongoza kwa goli 1-0 mpaka dakika za lala salama, lakini magoli la Teddy Sheringham na Gunnar Solskjær yaliwapa Manchester United taji la pili la UEFA.
Bayern walikuwa tayari wakijiandaa kushangilia ushindi lakini mambo yalivyobadilika ghafla ama hakika mashabiki, wachezaji mpaka viongozi walimwaga machozi uwanjani.
Contacts:
E-mail: - mwamunyimalecela@gmail.com
Facebook:- malecela mwamunyi
Google+:- malecela mwamunyi
whatsapp:- 0758427270
No comments:
Post a Comment