• Breaking News

    Friday, May 13, 2016

    MICHEZO: FAINALI CHAMPIONS LEAGUE NA EUROPA LEAGUE BUUUREE NDANIYA YOUTUBE

    Kuangalia mechi live kupitia TV zetu ni jambo la gharama sana, na ndio maana shirikisho la soka la barani ulaya UEFA limechukua maamuzi ambayo huenda yakakufurahisha wewe mpenzi wa soka kuelekea fainali za michuano ya Champions League na Europa League.

      Kwa mujibu wa BBC, fainali za michuano hiyo ya ulaya zitaoneshwa live kupitia mtandao wa YouTube. 

    Warusha matangazo ya live ya mechi za ulaya, kampuni ya BT Sport ya Uingereza wataonesha mechi hizo kwenye channels zao na pia kwenye mtandao wa YouTube. 

      Kikosi cha Jurgen Klopp cha Liverpool kitakutana na mabingwa watetezi Sevilla katika fainali ya Europa, jumatano ya tarehe 18 May, wiki ijayo. 

      Mahasimu wa La Liga  Real Madrid na Atletico Madrid watafuatia kwa kukutana kwenye fainali ya mabingwa wa ulaya, Jumamosi ya tarehe 28 May. 

    Liverpool ambao mashabiki wao wengi watashindwa kusafiri kwenda Basel kushuhudia fainali, wameamua kuonyesha live mechi hiyo katika eneo la Echo Arena, ambalo lina uwezo wa kuingiza watu 9,000 waliokaa. 

      Mnamo mwaka 2013, BT Sport walitangaza dili la miaka 3 lenye thamani ya £897m kuonyesha mechi zote 350 za michuano hiyo ya Champions League na Europa kuanzia mwaka 2015. 

    Katika moja ya sehemu ya mkataba huo, BT ilisema kwamba itaonyesha bure japo mchezo mmoja ambao utahusisha timu kutoka England kwa kila msimu. 

    No comments:

    Post a Comment

    PAGES

    AUDIO (5) General (1) HABARI (6) michezo (11) UDAKU (1)