• Breaking News

    Thursday, May 12, 2016

    FAHAMU MADHARA YA KUKOSA USINGIZI

    Wanasayansi wanaamini kuwa wamepata sababu moja mpya ya kwa nini tunahitaji usingizi,kutokana na utafiti huo unaonesha kulala kunasaidia katika kujenga seli mpya za ubongo,ambazo hujenga kemikali inayojulikana kama ‘Myelin’ ambayo ni muhimu katika kulinda ubongo wetu kwa ambavyo unafanya kazi.

    Pamoja na utafiti huo lakini kuna baadhi ya watu hudhani kwamba kulala usingizi ni kupoteza wakati, kwa upande mwingine, wengine hutamani sana kupata usingizi mtamu lakini hujigeuza-geuza kitandani hadi asubuhi.

    Kwa nini baadhi ya watu hushindwa kulala, hali wengine wanatamani sana kuwa macho? Je, tuuone usingizi kuwa starehe tu au ni muhimu? Ili kujibu maswali hayo, ni lazima tufahamu umuhimu wa usingizi

    MADHARA YA KUKOSA USINGIZI

    Kukosa usingizi huwezesha mwili kuharibu kemikali ambazo inasemekana zinasababisha kansa na kufanya chembe zizeeke. Katika uchunguzi wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo Kikuu cha Chicago, wavulana 11 wenye afya waliruhusiwa kulala kwa muda wa saa nne tu kwa siku sita.

    Kukosa usingizi husababisha kisukari kwani kiwango cha insulini kwa mwanadamu ambaye anapata usingizi mdogo huwa kama mtu ambaye anao ugonjwa wa kisukari kwenye damu yao kilikuwa kama kile cha mtu mwenye ugonjwa wa sukari!


    Kukosa usingizi huathiri pia utengenezaji wa chembe nyeupe za damu na homoni iitwayo ‘cortisol’, jambo ambalo humfanya mtu apate maambukizo na magonjwa ya damu kwa urahisi.

    Imetahadharishwa kwamba kulala usingizi wa chini ya saa 6 kila usiku kunaweza kusababisha mtu apatwe na kifo cha mapema. Watafiti wamesema watu ambao kwa kawaida huwa wanalala masaa hayo machache wengi wao hupatwa na vifo vya mapema kwa asilimia 12 zaidi ya wale wanaolala kawaida kwa masaa 8. Vifo ambavyo hutokea katika umri wa baada ya miaka 25. Pia imeonyeshwa kwamba kulala zaidi ya saa 9 kunapelekea vifo vya mapema ingawa kulala huko kunaweza kukawa na uhusiano na matatizo ya kiafya. Utafiti huo umetolewa kwa kuchunguzwa uhusiano uliopo kati ya kifo na usingizi kwa kutegemea chunguzi 16 zilizofanywa kwa kuwahusisha watu milioni 1 na nusu katika nchi za Uingereza, Marekani , Ulaya na Mashariki mwa Asia

    No comments:

    Post a Comment

    PAGES

    AUDIO (5) General (1) HABARI (6) michezo (11) UDAKU (1)