Ukiulizwa kiungo bora duniani kila mtu atakua na jibu lake kutokana na jinsi anavyofikiri ama aliyoyaona akiyafanya uwanjani. Kwa hapa Bongo wengine watamtaja Haruna Moshi wengine, Salum Aboubakari na Haruna Niyonzima ama Mwinyi Kazimoto lakini yote hiyo ni katika kujua utamu wa soka na mafundi wa kulisakata soka. Nani kama Andres Iniesta?
ANDRES INIESTA NI NANI?
Alizaliwa katika kijiji cha Fuetealbilla jimbo la Albaacate 11 May 1984 kwa sasa ana miaka 31. Ana vaa jezi namba 8,ameoa July 8 2012 na ana mtoto mmoja wa kike aitwaye Valeria. Sifa kuu ya Iniesta akiwa uwanjani na kwenye maisha ya kawaida ni aibu na upole.
AMEFANYA NINI KATIKA MPIRA?
Iniesta alianza maisha ya soka La Masia alicheza Barcelona B, jumla ya michezo 54 na kufunga magoli 5. Alipandishwa hadi Barcelona ya wakubwa mwaka 2002, abapo hadi sasa amecheza michezo 387 amefunga magoli 34. Kwa upande wa timu ya taifa amecheza michezo 107 na kufunga magoli 13. Amewekeza katika timu yake ya mtaa inayoitwa ALBACETE iliyokuwa inashiriki ligi daraja la pili lakini baadae ikashuka daraja.
Ameingia mara tatu kwenye tatu bora ya mchezaji bora wa Dunia hajawahi kuchukua na mara zote alichukua mchezaji mwennzake Lionel Messi. Mwaka 2010 alichukua uchezaji bora wa Ulaya. Anasifika kwa kufunga magoli ya mhimu kwenye klabu yake ya Barcelona na Timu ya taifa ya Hispania likiwemo bao kwenye fainali ya kombe la dunia 2010 dhidi ya Uholanzi nchini Afrika Kusini. Iniesta Amechukua makombe yote ulimwenguni kama ilivyo kwa Thiery Henry.
No comments:
Post a Comment