• Breaking News

    Friday, May 20, 2016

    SAMATTA: NIMEJIFUNZA KITU KWENYE FAINALI YA EUROPA


    Samatta-Nape 4
    Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta anaecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Genk nchini Ubeligiji amesema amejifunza jambo kwenye mchezo wa jana wa fainali ya Europa League kati ya Liverpool dhidi ya Sevilla.
    Samatta anasema kikubwa alichojifunza na kilichomfurahisha ni namna ambavyo Sevilla waliweza kutoka nyuma kwa golin 1-0 na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 na hatimaye kunyakua kombe la Europa kwa mara ya tatu mfululizo.
    “Mechi ya jana kitu kilichonifurahisha ni namna ambavyo Sevilla walivyorudi kwenye game baada ya kuwa wako nyuma kwa goli 1-0, ni kitu kizuri kwa timu na mchezaji. Baada ya kuwa mko chini kwa goli halafu mnarudi kupata ushindi katika mechi ya fainali ni kitu ambacho kinapendeza”, anasema Samatta ambaye leo ameanza kwenye kikosi cha kwanza kinachocheza mchezo wa play off dhidi ya Anderlecht.
    Katika mchezo wa fainali ya jana kati ya Liverpool na Sevilla, Liverpool walianza kupata bao la kuongoza dakika ya 35 lakini baadaye Sevilla walisawazisha bao hido dakika ya kwanza baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kisha kuongeza magoli mengine mawili na kushinda mchezo huo wa fainali.

    No comments:

    Post a Comment

    PAGES

    AUDIO (5) General (1) HABARI (6) michezo (11) UDAKU (1)