• Breaking News

    Tuesday, May 31, 2016

    TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA



    1.CHELSEA {EPL}
    Beki wa kulia wa timu ya Juventus Stephan Lichtsteiner anatakiwa Chelsea itatokea pale beki wa Barcelona Dani Alves pindi atakapowasili klabuni hapo na Antonio Conte anaonekana kuhitaji huduma ya mchezaji huyo, unaweza ukajiuliza Baba Rahman na Ivanovic watacheza wapi? hilo sio lako muachie Conte.
    2.INTER MILAN {SERIE A}
    Uongozi wa Inter Milan haujathibitisha juu ya ujio wa nyota wa Sevilla Ever Banega lakini mshangao ni kwamba mchezaji nyota wa zamani wa timu hiyo Javier Zanetti  ametangaza kuwa nyota huyo wa Sevilla tayari amesainiwa na timu hiyo.
    3.BARCELONA {LA LIGA}
    Kiungo wa Manchester United ambaye kitaaluma ni Mwandishi wa Habari na ana “Degree” ya uandishi wa habari Juan Mata anaweza kuondoka klabuni hapo mara baada ya ujio wa kocha ambaye amemtosa wakati yupo Chelsea JOSE MOURINHO. Barcelona wako karibu kufuatilia filamu hii endapo watamuweka sokoni wapo tayari kuulizia bei, ingekuwa wanazungumza kifaransa wangesema “Deja vu” kwa maana kuelezea hisia za mtu.
    4.REAL MADRID {LA LIGAl}
    Wakala wa nyota wa Bayern Munich Robert Lewandowski anayefahamika kwa jina la Cezary Kucharski amesema kuwa Real Madrid wametuma maombi kwa nyota huyo na wako katika mazungumzo.
    5.BORRUSIA DORTMUND { BUNDESLIGA}
    Baada ya uvumi kuwa kiungo wao  Gundogan kutakiwa Manchester City timu hiyo inaanda mpango mbadala wake ambapo sasa wanataka kuibomoa Bayern Munich kwa kiungo Sebastian RODE.

    No comments:

    Post a Comment

    PAGES

    AUDIO (5) General (1) HABARI (6) michezo (11) UDAKU (1)