Chama cha soka nchini Argentina (AFA) kimetishia kuitoa timu yake ya taifa nje ya mashindano ya Copa America kutokana na serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka.
Argentina ni miongoni mwa timu ambazo zinapewa nafasi kubwa ya kuibuka bingwa wa michuano hiyo itakayofanyika Marekani na June 7 wanatarajia kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya mabingwa watetezi Chile kwenye mji wa Santa Clara, Califonia.
Lakini ushiriki wao umeingia mashaka baada ya AFA kuingia kwenye mgogoro na serikali ya Argentina kufuatia serikali kuusimamisha uchaguzi wa rais wa chama hicho kinachosimamia soka la Argentina ambao ulipangwa kufanyika June 30 huku wakiteuliwa ma-inspectors kuchunguza tuhuma za mapato ya TV ambazo zinalikabili shirikisho hilo.
Katibu mkuu wa AFA Damian Dupiellet amekiambia kituo kimoja cha redio nchini humo kwamba, bodi ya mkutano wa dharura itaamua kama timu ya taifa ya Argentina itarudishwa nyumbani kutoka Califonia ambako inaendelea na maandilizi kuelekea mashindano hayo.
“Uchaguzi umesogezwa mbele kwa siku 90 na huenda ukasogezwambele kwa siku 90 nyingine tena”, amesema Dupiellet, Katibu Mkuu wa AFA. “Ma-Inspector wawili wameteuliwa kufanya uchunguzi ndani ya AFA. Huku ni kuingilia moja kwa moja masuala ya AFA”
FIAFA imezisimamisha nchi kadhaa miaka ya hivi karibuni kutokana na serikali zao kuingilia masuala ya soka ambazo ni pamoja na Nigeria, Cameroon na Indonesia, huku Dupiellet akiongeza kusema “Tutaomba ufafanuzi toka CONMEBOL na FIFA kufanya upembuzi kama suala hili ni kinyume na kanuni za mashirikisho hayo.
Taarifa kutoka kitengo cha upelelezi (Inspeccion General de Justicia) ndani ya Wizara ya Haki ya Argentina kuuzuia uchaguzi huo zilithibitishwa na taarifa kutoka tovuti AFA.
Gazeti la Clarin limeripoti kwamba, matumizi mabaya ya pesa ndani ya AFA ni sababu kubwa iliyopelekea serikali kuingilia na kuupiga stop uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment