• Breaking News

    Wednesday, June 1, 2016

    WOLPER ADAI KUFILISIWA NA MKONGO


    Msanii wa filamu, Jacqueline Wolper baada ya kukiri kwamba anatoka kimapenzi na Harmonize, amefunguka na kueleza madai ya kufilisiwa na Mkongo ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani.

    Akiongea katika promo ya kipindi kipya cha Take One ambacho kinatarajiwa kuruka Jumanne hii, Wolper amedai yeye ndiye aliyetendwa na Mkongo ambaye alikuwa mpenzi wake, kwani wakati anaanza naye mahusiano alikuwa ana gari na nyumba lakini baadae akijikuta hana hata sehemu yakulala.

    Muigizaji huyo ambaye amekuwa akionyesha uwezo mkubwa katika filamu zake, amedai alikuwa anajilipia nyumba kwa dola, lakini ulifikia wakati akafilisika na kuanza kulala hoteli.

    Wolper amedai mahusiano hayo yalimsababishia kugombana na baadhi ya watu wake wa karibu ambao walikuwa wakimshauri vizuri, lakini yeye alikuwa akiwaaona kama wanamfitini.

    Muigizaji huyo ambaye amewahi kutamba na filamu yake Tom Boy, kwa sasa anatoka kimapenzi na hit maker wa wimbo ‘Bado’, Harmonize kutoka WCB.

    No comments:

    Post a Comment

    PAGES

    AUDIO (5) General (1) HABARI (6) michezo (11) UDAKU (1)