• Breaking News

    Saturday, June 4, 2016

    SKY SPORTS WAMETOBOA HII KUHUSU ZLATAN IBRAHIMOVIC NA MAN U



    Najua wewe ni mmoja kati ya watu wanaojiuliza maswali nahodha wa timu ya taifa ya SwedenZlatan Ibrahimovic atacheza klabu gani msimu ujao, basi majibu yanakaribia kupatika hasa baada ya Sky Sport kuripoti kuwa staa huyo yupo njiani kujiunga na klabu ya Man United.
    Sky Sport wameripoti kuwa Zlatan atakamilisha usajili wa kujiunga na Man United wakati wowote kuanzia sasa ila ni kabla ya michuano ya mataifa ya Ulaya kuanza, Sky Sportwanaeleza kuwa kocha wa Man United Jose Mourinho amepanga kusajili mshambuliaji mmoja katika dirisha hili la usajili ila Zlatan Ibrahimovic ndio chaguo lake.
    Mtendaji mkuu wa Man United Ed Woodwardna wawakilishi wa Zlatan wanaripotiwa kuwa katika mazungumzo ya mwisho ili kumsajili staa huyo kwa mkataba wa mwaka mmoja, Zlatankwa sasa yupo na timu yake ya taifa yaSweden anajiandaa mchezo wao wa kwanza wa Euro 2016 dhidi ya Ireland utakaochezwa June 13.

    No comments:

    Post a Comment

    PAGES

    AUDIO (5) General (1) HABARI (6) michezo (11) UDAKU (1)