Beki wa kulia wa Barcelona Dani Alves, ameitumikia klabu hiyo kwa takriban miaka nane na sasa anaondoka rasmi msimu huu na anatarajia kujiunga na miamba ya Serie A Juventus kwa mkataba wa miaka miwili.
Akiwa na Barcelona, Dani Alves (33) ameshinda makombe 23, yakiwemo mtatu ya Champions League na sita ya La Liga.
Beki huyo aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kusaidia mashambulizi ameacha ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa Instagram, maalum kwa ajili ya mshabiki wa Barcelona.
Ujumbe unasomeka hivi:
“Umebaki mwezi mmoja tu kutimiza miaka nane tangu nijiunge na klabu hii ya Barcelona. July mwaka 2008 ndiyo muda niliojiunga na klabu hii na nimeweza kuitumia jezi hii maridadi kukamilisha ndoto zangu nyingi katika maisha ya soka. Kunzia siku ya kwanza, nikiwa nafanya mazoezi kwa mara ya kwanza chini ya Pep Guardiola, mpaka mwisho wa msimu huu, nimekuwa ni mwenye bahati kubwa na kufurahia maisha yangu ya soka”.
“Nina dazeni, mamia ya matukio ambayo ni kumbukumbu kubwa sana kwangu ambazo nime-share hapa Camp Nou na mitaa mbalimbali ya jiji la Barcelona…tumesherehekea magoli mengi sana, na furaha wakati tukiwa tumeshinda mataji. Heshima na uchapakazi wangu kwenye soka umenifanya nivae moja ya jezi za klabu bora duniani kwa takriban muongo mmoja kutokana na ubora wa wachezaji na makocha wake”.
“Ningeweza kuwataja mmoja mmoja wote ambao nimefanya nao kazi kwenye furaha na changamoto kwa kipindi chote nilichodumu klabuni hapa, lakini ningependa kuwashukuru kwa pamoja, kwasababu kwenye familia ya Barcelona hakuna nafasi ya ubinafsi: Tunafungwa pamoja, tunashinda pamoja na tunafanya kazi kwa pamoja kwa msaada wa Marais, mameneja na wafanyakazi wengine kwenye klabu….wote kwa pamoja nawashukuru sana kwa sapoti na imani yao kubwa kwangu kutokana na kutambua na kuthamini mchango wangu”.
“Nimeandika barua hii kwa sababu nataka kuwajulisha kwamba nimefanya maamuzi haya kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya katika maisha yangu ya soka, kwasababu nyote mnapaswa kujua kwamba kila hatua katika maisha ina maana kubwa sana. Na maana yangu ni kwamba. Naondoka lakini nitarejea. Asante sana kwa upendo wenu wa dhati”.
No comments:
Post a Comment