• Breaking News

    Sunday, June 5, 2016

    UKWELI WA VARDY KUJIUNGA NA ARSENAL HUU HAPA

    Arsenal vs Leicester
    Dili la Jamie Vardy kujiunga na Arsenal kwa mara ya kwanza lilitangazwa usiku wa Ijumaa June 3 na sasa mambo yanakaribia karibia.
    Kwa mujibu wa mtandao wa goaltayari mipango imeshaandaliwa kwa ajili ya vipimo vya afya vya Vardy leo Jumapili na kila kitu kinakwenda kwenye mstari. Dili hilo linatarajiwa kukamilika Jumatatu kabla ya kikosi cha England hakijapaa kwenda Ufaransa kwa ajili ya fainali za Euro mwaka 2016.
    Kocha wa Leicester Claudio Ranieri amethibitisha kupitia vyombo vya habari vya Italy kwamba kila kitu kinakwenda sawa na inaonekana dili hilo ni halali.
    Vyanzo mbalimbali vimeripoti kwamba, bila shaka lolote Vardy anatua Arsenal kwa dau la £20million.
    Vardy ambaye alijiunga na Leicester kwa ada ya uhamisho kiasi cha £1m kutoka Fleetwood mwaka 2012, alimaliza ligi akiwa nafasi ya pili kwa ufungaji baada ya kufumania nyavu mara 24 na kuisaidia timu yake kushinda taji la EPL msimu wa 2015-16.

    No comments:

    Post a Comment

    PAGES

    AUDIO (5) General (1) HABARI (6) michezo (11) UDAKU (1)