• Breaking News

    Friday, May 20, 2016

    MICHEZO: TAKWIMU KUTHIBITISHA UBORA WA LA LIGA DHIDI YA LIGI NYINGINE ULAYA

    Ushindi wa 3-1 wa Sevilla vs Liverpool kwenye fainali ya Europa League _ huku Real Madrid na mahasimu wao Atletico Madrid wakitegemewa kucheza fainali ya Champions League wiki ijayo – timu za Spain zimeshapata uhakika kutwaa makombe yote ya ulaya kwa msimu mwingine. 
      Hii itakuwa mara ya 3 mfululizo kwa vilabu vya La Liga kushinda makombe yote mawili ya ulaya. 
    Katika timu 13 za mwisho kushinda Europe League – 8 kati hizo zimetoka nchini Spain katika La Liga – Huku Sevilla wakiwa washindi kwa mara 5. 
    Wakati ubingwa wa Champions League  wa msimu huuutaenda aidha kwenye klabu moja au nyingine ya Spain wakati mahasimu wa jiji la Madrid watakapokutana mwishoni mwa wiki hii jijini Milan katika dimba la San Sirro.
      Magoli Ivan Rakitic, Luis Suarez na Neymer waliiongoza Barcelona kuifunga Juventus 3-1 jijini Berlin kwenye fainali ya UCL mnamo May  2015 — huu ulikuwa ushindi wa 3 baada ya kuwafunga Manchester United katika fainali za msimu wa 2009 na 2011.
    Wakafuatiwa na Real Madrid  ya Carlo Ancelotti ambao waliwafunga wapinzani wao Atletico Madrid misimu miwili iliyopita baada ya mchezo kwenda mpaka dakika za nyongeza 30 na magoli ya  Ramos, Gareth Bale, Marcelo na Cristiano Ronaldo kubadili mchezo.
      Hakuna nchi ambayo imewahi kuwa na utawala wa kiasi hiki katika soka la ulaya. 
    Kipigo cha Valencia mbele ya Bayern Munich mnamo 2001 ndio kilikuwa kipigo cha mwisho kwa timu ya Spain kutoka kwa timu ya taifa lingine katika mchezo wa kuamua bingwa wa michuano mikubwa ya ulaya. 

    Mafanikio ya vikombe kwa timu za Hispania tangu mwaka 2014

     Tangu mwaka 2001, vilabu vya Spain vimeshinda fainali 13 – hapo bila kutaja makombe mawili ya Euro na Moja la kombe la dunia waliloshinda timu yao ya taifa. 

    No comments:

    Post a Comment

    PAGES

    AUDIO (5) General (1) HABARI (6) michezo (11) UDAKU (1)